Mbinu hii ni muhimu katika kujua fursa zinazokuzunguka


Nikiwa kama mhenga mpya naomba nikuongezee msemo huu mpya usemao "Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili". Mara nyingi ugumu wa maisha hutokea ili kupima imani zetu juu ya kupambana na maisha pamoja na changamoto zake. 

Changamoto zinazojitokeza katika maisha yetu ya kila siku huwa na sababu zake za msingi. Mosi sababu ya kutokea katika changamoto hutokea ili kupima una uvimilivu kiasi gani juu ya kupambana na changamoto. 

Lakini sababu ya pili ni kwamba mara nyingi changamoto zinazojitokeza katika maisha ili kupima matumizi yetu ya jicho la tatu. 

Na katika matumizi ya jicho la tatu ndilo ambalo nitalizungumzia zaidi, hii ni kwa sababu watu wengi pindi zitokeapo changomoto fulani huwa ni wepesi sana wa kukata tamaa kuliko kutumia jicho la tatu katika kuzitatua changamoto hizo. 

Lakini pia jicho la tatu kazi yake kubwa huwa ni kuona changamoto katika upande wa fursa zaidi. Pia ikumbukwe kama utaamua kulitumia jicho hili la tatu kutakusadia sana kuweza kuona fursa nyingi zinazopatikana eneo ambalo unaishi. 

Kila palipo na changamoto pana fursa hivyo unatakiwa kutumia jicho la tatu katika suala la kung'amua fursa mbalimbali zitokanazo na changamoto husika. 

Mwisho niweke nukta kwa kusema changamoto zilizopo katika jamii yako ndiyo fursa ambazo zimejaa kila kona hivyo unatakiwa kutafutia majibu ya changamoto hizo. Hivyo jifunze kuzibadili changamoto ziwe fursa kila wakati. 

No comments

Powered by Blogger.