Ronaldo amkana mwanamke aliyesema amembaka, " Wanataka umaarufu'



Cristiano Ronaldo ametupilia mbali madai ya mwanamke mmoja nchini Marekani ambaye anadai kuwa staa huyo wa Juventus alimbaka mwaka 2009. 

Kwenye video ya Instagram Ronaldo alisema: "Wanataka umaarufu kwa kutumia jina langu. Hiyo ni kawaida." 

Mawakili wa Ronaldo wanasema wanalishtaki jarida la Ujerumani la Der Spiegel lililoripoti kwanza madai hayo. 

Jarida hilo lilindika kuwa Kathryn Mayorga alikuwa amedai Ronaldo 33, alimbaka kwenye chumba kimoja cha hoteli huko Las Vegas. 

Bi Mayorga, 34, anaripotiwa kuandika taarifa ya kubakwa kwa polisi wa Las Vegas muda mfupi baada ya kisa hicho. 

Mwaka 2010 anaripotiwa kufikia makubaliano na Ronaldo ya malipo ya dola 375,000 ili asifichue madai hayo. 

Mawakili wake sasa wanataka makubaliano ya kutofichua madai hayo yatupiliwe mbali. 

Ronaldo alijiunga na Juventus ya Italia kwa pauni milioni 99.2 akitokea Real Madrid mapema mwaka huu. 

Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kipindi hiki duniani.

No comments

Powered by Blogger.