Yanga yaanza vibaya makundi
WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga wameanza vibaya hatua ya makundi baada ya kufungwa mabao 4-0 na USM Algers leo Jumapili.
Katika mchezo huo wenyeji walionekana kutawala na kutengeneza nafasi nyingi za mabao tofauti na Yanga ambao walionekana kucheza kwa kujilinda zaidi.
Kasi ya wenyeji ilizaa matunda mapema dakika ya nne baada ya kupata bao la kuongoza kupitia kwa Darfalou Oussama aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Rafik Boudebal.
Wenyeji waliendelea kulisakama lango la Yanga kama nyuki na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 32 lilolofungwa na Chafal Farouk.
Mabao hayo mawili yalidumu hadi mapumziko na dakika tisa tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Abderahmane meziane aliwapatia wenyeji bao la tatu kwa shuti kali nje ya eneo la hatari.
Wakati kila mmoja akiamini mechi hiyo itamalizka kwa matokeo hayo, kipa Mohammed Zemmamoche aliwapatia wenyeji bao la nne kwa mkwaju wa penati iliyotolewa dakika za nyongeza baada ya Andrew vincent kumfanyia faulo mmoja wa wachezaji wa USM Alger

Post a Comment