TFF yasikitishwa na Yanga


Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umekanusha taarifa zilizotolewa na Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini, Bakili Makele akieleza kuwa wanalidai Shirikisho hilo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 200. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Matawi ya Yanga nchini, alieleza kuwa wanaidai TFF zaidi ya fedha hizo milioni 200 kutokana na kuikata mapato baada ya kuingiza mashabiki bure katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Juni 18 2016, vilevile ikiwemo fedha za mchezo uliopita kati ya Simba na Yanga. 

Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amekanusha taarifa hizo huku akisema Yanga wamemtumia kiongozi huyo wa matawi kuzungumza wakati hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo. 

Ndimbo amesema kuwa Yanga wanajua kila kitu kuhusiana na deni hilo na hawakuwa na sababu ya kumtumia mtu ambaye hafahamu chochote kuhusiana na suala hilo hivyo watapaswa kutoa majibu ya kwanini wamemtumia. 

Mbali na hilo, Ndimbo amesema pia kuwa ni kweli walizuia fedha zao za mapato zilizopatikana katika mchezo wa Simba na Yanga kutokana na deni ambalo wao wanadaiwa hivyo ikabidi wawakate. 

Mwisho Ndimbo ameeleza kuwa TFF inaidai Yanga hivyo huku akieleza imesitikishwa na malalamiko ya mtu ambaye hakuwa na mamlaka ya kulisemea suala hilo wakati Yanga wanajua kila kitu.

No comments

Powered by Blogger.