Ozil atupiwa lawama na Wachezaji wa Arsenal
Mesut Ozil ni moja kati ya majina makubwa katika Ligi Kuu England kwa sasa hususani katika club ya Arsenal kwani yeye ndio mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi ya wachezaji wote wa Arsenal.
Jina la kiungo wa Ujerumani linazidi kuchukua headlines kufuatia stori zinazoripotiwa katika mitandao kuwa Mesut Ozil amekuwa na tabia ambayo sio nzuri licha ya kuwa ndio mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi ya wachezaji wote wa Arsenal.
Wachezaji wa Arsenal wanadaiwa kuhoji tabia ya Ozil na kudai kuwa hajitoi kwa kiasi kikubwa katika timu ukizingatia amekosekana katika game 5 za Arsenal zilizopita na sasa inaripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu hadi Kombe la Dunia litakapoanza.
Inaripotiwa kuwa Ozil anayelipwa mshahara wa pound 350000 kwa wiki licha ya kuwa anatajwa kuwa nje ya uwanja kwa majeruhi, wenzake wanaona tabia ya Ozil kudai kuwa na majeruhi ni kama tabia ya kuchagua mechi za kucheza kwani katika game 58 za Arsenal msimu huu Ozil ameanza katika game 25 pekee.
Kwa upande wa kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonekana kutoa kauli za kumtetea “Mchezo wa mpira hauko hivyo na sio kama anachagua mechi bali ni majeruhi madaktari wameniambia kuwa ni hatari kumchezesha kwa sasa itakuwa ni hatari sana kujaribu kumtumia akiwa hayupo fiti”
Post a Comment