Familia moja jijini Dar yapaza sauti kwa JPM, yadai kudhurumiwa


Familiya moja iliyokuwa ikiishi barabara ya Mfaume, Kata ya Upanga Mashariki, jijini Dar es Salaam wamepaza sauti na kilio kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Mkoa huo Paul  Makonda kuwasaidia  kupata haki yao amabayo inaonekana kuporwa. 

Akizungumza na wanahabari leo msemaji wa familia hiyo Bi. Edith Max ameeleza kuwa awali mume wake ambaye anatambulika kwa jina la Emmanuel Max alikopa fedha katika benki ya Furaha ambapo benki hiyo ilibadilishwa jina kwa sasa inafahamika kama I &M Bank, ambapo kiasi cha fedha zilizokopwa ni shilling million 30 lakini anadai walikatazwa kulipa na baada ya hapo kuwatoa katika nyumba hiyo  kudai kuwa wameshindwa kulipa mkopo ambao ulipanda na kufikia deni la shillingi million 120. 

Ameendelea kusema kuwa walipotaka kulipa mkopo huo,waliambiwa wasubiri kwanza wataambiwa walipe baadae ya hapo walikwenda kwa ajili ya kulipa ndipo walipoambiwa kuwa Riba imeongezeka hivyo watatakiwa kulipa kiasi cha shilling million 90. 

"Tulipoambiwa tulipe million 90, Mume wangu alikubali na akawa tayari kwa ajili ya kulipa lakini alipokwenda kulipa wakamwambia asubiri mwezi mmoja alafu watatuita baadae ya mwezi kwisha tukaenda kwa ajili ya kulipa wakasema Ribs imepanda Ivyo tunatakiwa kulipa million 120, tukawa tuko tayari kulipa na tunafanya mchakato wa kulipa" ameeleza. 

Ameendelea kusema' Tukiwa tunafanya mchakato wa kulipa tukaja kutolewa katika hii nyumba mwaka 2014 na watu wakidai kuwa tumeshindwa kulipa mkopo huo jambo ambalo sio kweli kutokana na kuna kuondolewa kwa ghafla hali hiyo ilisababisha mama mkwe wangu kupata presha na kufariki na kupelekea mume wangu kupooza jambo lililopelekea Mimi kuahangaika na familia pekeangu na huku nina watoto wanne" 


Amesema walibaini udanganyifu unaofanywa na Benki hiyo kwani kila wakitaka kulipa deni wanaambiwa wasubiri na baada ya hapo waligushi vyeti vya mirathi feki na hakuna mwanafamilia yeyote alietambulika katika mirathi hiyo. 


Aidha Bi. Max amesema Familia  ili fungua Mirathi yake tarehe 17 Januari katika  Mahakama ya  mwanzo Kinondoni na Msimamizi wa Mirathi hiyo Max Edmund Kafipa. 

Amesema awali suala hili walilipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Kampeni yake  ya kuwa sikiliza walidhulumiwa nyumba, viwanja na Mashamba  ambapo walifika katika ofisi hizo January 30, mwaka huu.ambapo pande zote ziliitwa na kujadiliana kwa wanasheria na maamuzi yao yanatarajiwa kutolewa  tarehe 7 May 2018. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Abdulkarum Gulam Shambe, amesema ni kweli kuwa jambo hilo lipo na mgogoro huo kati yao na benki na kwamba taarifa za kuvunjwa kwa nyumba hiyo alipata  baada ya kuanza kuvunja ndipo walipopeleka taarifa hizo kwake.

No comments

Powered by Blogger.