WHO yarekodi kiwango cha juu cha maambukizi kwa siku
Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema jana kwamba limesajili rekodi mpya ya siku ya visa vya COVID-19, wakati idadi ikakaribia kwa haraka katika kiwango cha kutisha cha maambukizi milioni tano.
Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Gebreyesus amesema kupitia twitter siku ya Jumanne kwamba kulikuwa na visa 106,000 vilivyoripotiwa kwenye shirika hilo, idadi ya juu kabisa tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Disemba.
Shirika hilo linaendelea kukabiliwa na shinikizo baada ya rais Donald Trump kulipatia siku 30 za kujirekebisha, na likishindwa kufanya hivyo, Marekani ambayo ni mchangiaji mkubwa itaondoa ufadhili wake na kujiondoa uanachama moja kwa moja.
Tedros amewaambia waandishi wa habari bado kuna safari ndefu na shirika hilo limeonya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi katika mataifa masikini.

Post a Comment