Yafahamu mavazi mazuri kwa Wanawake wanene

Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiangaika kupata aina ya nguo za kuvaa tena hasa wanawake wanene, kutokana na maumbo yao wanaona ni kazi sana kutafuta nguo, wengine hukosa hata uhuru wa kutoka out na watu wao wa karibu kwa sababu tu wanakosa nguo.Wengi ujikuta wakichagua nguo pana pana ili kuficha maumbo yao, lakini kumbe unaweza kuwa huru sana na mwili wako. 

Zifuatazo ni badhi ya tips zinazoweza kukusaidi kuchagua nguo za kuvaa kwa mwanamke mnene.Inawezekana nguo hizi unazo ndani lakini unashindwa kuzipangilia; 

1. Kabla ya kuchagua nguo ni lazima kujua mwili wako una unene wa aina gani,ikiwa wewe ni mnene na unatumbo kubwa basi ni bora kuvaa gauni maana gauni uweza  kukuweka vizuri na pia ni mazuri hasa kwa watu wanene. 

 2. Lakini pia kama wewe ni mnene na umebahatika kuwa na maziwa makubwa, ni vizuri kupendelea kuvaa nguo zenye v-shape, siri ya nguo hizi ni kwamba huwa na tabia ya kuficha ukubwa wa maziwa na kufanya uwe maridadi zaidi ila zingatia kuchagua brazia nzuri kuikaa blauzi yako sawia. 

3. Kwa mwanamke mwenye hipsi anashauriwa kuvaa nguo zinakazo mfanya hasionyeshe sana hipsi zake tofauti ya yule hasiekuwa na hipsi , maana yeye anatakiwa kuvaa nguo itakavyo onyesha hipsi zake , hata hivyo kwa wanawake wanene wenye hipsi hawana haja ya kujibana sana kwa sababu hipsi huweza kujitokeza zenyewe tu. 

4. Lakini pia kuchagua rangi ya nguo  nzuri pia husaidia kupunguza au kuongeza umbile la mtu, kuna rangi huweza kukufanya ukawa mnene sana au mwembamba sana,kwa mfano  nguo zenye mistari ya kulala sio nzuri kwa watu wanene maana hutanua miili yao.Lakini pia rangi za giza hupunguza muonekano wa unene ilihali rangi za mwanga huangaza na kufanya mtu aonekane sana. 

Zingaia: 
-Ni bora zaidi katika kuchagua rangi nguo za rangi nyeusi na nyeupe iliyochanganywa ni nzuri zaidi inafanya muonekano wa mtu uonekane maridadi zaidi. 

-Lakini pia jitahidi kuvaa viatu vinavyoendana na mwili wako ,sio lazima kuvaa kiatu kirefu wakati mwili wako hauimili mikikimikiki ya kiatu kirefu, flatshoes pia hupendeza zaidi kwa mtu mnene .

No comments

Powered by Blogger.