Tanasha wa Diamond mjamzito?


Kila kukicha kwenye mitandao ya kijamii hakuishi maneno na mitazamo tofauti tofauti juu ya watu mbalimbali hasa wale watu mashuhuri. 

Mpenzi wa Mwanamuziki Diamond, Tanasha Donna huenda akawa mjamzito baada ya kutuma kipande cha video katika mtandao wa Instagram akiwa na mpenzi wake wakiicheza wimbo mpya  aliomshirikiana na msanii kutoka nchini Congo, Fally Ipupa huku tumbo likionekana kubwa tofauti na alivyokuwa awali. 

Hivi karibuni kumekuwepo na maoni ya watu tofauti katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakisema huenda Tanasha akawa mjamzito baada ya  picha anazotuma mitandaoni hivi karibuni kumuonesha akiwa na tumbo kubwa linaloonesha kukua siku baada ya siku. 

Japo wenyewe hawajathibitisha, endapo ikiwa ni kweli basi Diamond atakuwa anatarajia mtoto wa nne ikiwa anao watatu tayari ambapo  wawili (Latifa na Neelan) alizaa na Mwanamama Zarina Hassan ambaye ni raia wa Uganda na mtoto mmoja wa kiume (Dylan), aliyezaa na mrembo wa hapa nchini Hamisa Mobetto. 

No comments

Powered by Blogger.