Mambo yatakayokusaidia mwanamke kuongeza ladha katika mahusiano ya mapenzi

Hizi ndizo njia bora za kuongeza ladha katika mapenzi Itakuwa vyema kwako mwanadada kuhakikisha anamfanyia hivi mwanaume wa ndoto zako. 

Usimlinganishe na wengine. 
Hakuna mwanaume anayependa kulinganishwa na wanaume wengine katika mahusiano, kama uliyenaye unampenda kwa moyo wako wa dhati basi hakikisha ya kuwa unamuone yeye pekee. 

Yawezekana umekuwa na mchumba mmoja tu, ama yeye ni wa mia moja! Kwanza, usithubutu kumtajia idadi hiyo iliyowahi kuwa nayo. Pili, usimlinganishe hata chembe na hao wengine wa zamani isipokuwa tu kama yeye ndiye ameibuka bora kuliko wote. 

Usimkashifu Hakuna aliye kamili 
Hakuna mtu ambaye huwa anapendwa kukashifiwa hata siku moja, kila mwanaume anapenda heshima ichukue heshima yake. Ukiwa na tabia ya kumkashifu mumeo ujue fika mahusiano yako yanaelekea kuzama kama jua lifanyavyo. Hivyo kila wakati unatakiwa kujifunza kuwa kama unataka mahusiano yenu yawe ni yenye tija na yenye furaha ndani yake inatakiwa uepukane na tabia ya kumkashifu mpenzi wako. 

Acha kuishi kwa mazoea,  
Mpenzi wako ili aweze kukupenda kweli inatakiwa kuepukana na tabia ya kufanya vitu kimazoea, kama mpenzi wako amezoea kujipelekea maji bafuni basi unatakiwa kuanza kumpelekea maji kuanzia leo. Kama mwenza wako amezea kula mwenyewe basi unatakiwa kuanza kumlisha chakula kuanzia leo. 

Mtalamu mmoja wa mahusiano aliwahi kusema kuwa mwanaume ni kama mtoto mdogo, kwa sababu anapenda kudeka sana hivyo kila wakaji acha kufanya vitu kimazoea bali unatakiwa kumdekeza huyo mwenza wako. 

Usilete vita chumbani, Chumbani ni pahali pa kujituliza, kufungua roho yako na kujumuika pamoja na mpenzi wako kuleta raha. Chumbani ni sehemu tulivu kwenu katika kufanya mazungumzo yatayowaletea mafanikio ya kimaisha na mahusiano pia. Chumba chenu si sehemu ya kufanyia mitafaruko isiyokuwa na kichwa wala miguu bali sehemu nzuri sana ya kuwafanya mjenge mahusiano yenye mwanagaza wa maisha yenu. 

No comments

Powered by Blogger.