ETHIOPIA, Viongozi wa kidini wataka wapenzi wa jinsia moja wasiingie nchini

Muungano wa makanisa ya Ethiopia umeitolea wito serikali ya nchi hiyo kuzuwia mpango wa matembezi ya kampuni ya Marekani inayoandaa safari za wapenzi wa jinsia moja. 

Mungano huo wa makanisa ulikasirishwa hasa na taarifa ili iliyochapishwa na kampuni ya safari ya Toto Tours ambayo ilihusisha maeneo ya kidini nchini Ethiopia. 

Waethiopia wengi wanafuata dini sana na wanapinga suala zima la mapenzi ya jinsia moja , ambayo pia yanazuwiwa chini ya sheria za nchi hiyo. 

Mmiliki wa Kampuni ya safari ya Toto Tours ameiambia BBC kuwa kampuni ilikuwa imepokea vitisho na jumbe za chuki kwenye mitandao ya habari ya kijamii. 

" Sisi ni wanyenyekevu na tunawapnda watu , tunakuja na upendo akilini mwetu , hakuna tutatachofanya kitakachowadhuru watu, lakini tunachukuliwa kama watu wa madhara ," Dan Ware aliiambia BBC idhaa ya Amharic. 

Bwana Ware amesema kuwa anahofu na akaiomba wizara ya utalii ya Ethiopia "kuwa na uangalifu ". 

" Macho ya dunia yataelekezwa kwetu tutakapokuja na chochote kitakachofanyika kwetu katika utamaduni wa Ethiopia na sekta yake ya utalii." 

Wavuti wa Toto Tours unasema kuwa inapanga kufanya ziara ya kitalii nchini Ethiopia mwezi Oktoba mwaka huu . Miongoni mwa maeneo wanayopanga kutembelea ni pamoja na maeneo ya kidini kama vile Bahir Dar, kituo cha miujiza cha kikristo pamoja na Lalibela, eneo ambalo ni maarufu kwa kuwa na makanisa ya kale yaliyozungukwa na mwamba. 

Rais wa Muungano wa makanisa ya Orthodox-Selestu Me'et, ameiambia BBC kuwa serikali inapaswa "kulipiga marufuku kundi hilo lisiingie nchini na kutembelea maeneo matakatifu ". 

"hawapaswi kuruhusiwa kuacha alama zao ," alisema Bwana Dereje Negash . "Dini yetu inalaani kihtendo hiki , na ni cha laana." 

Alisisitiza kwamba mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria nchini Ethiopia , na akaongeza kuwa kampuni hiyo ya safari za kitalii haipaswi kuruhusiwa "kukiuka sheria ya nchi ". 

Bwana Negash pia ni Mkuu wa kanisa la Orthodox la Ethiopia ,na amekuwa akiendesha kampeni dhidi ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo. 

Wito kwa serikali wa kupiga marufuku kampuni hiyo uliungwa mkono na Muungano wa baraza la Dini mbali mbali wa Ethiopia, unaojumuisha madhehebu ya Kikristo na Kiislamu 

" Mipango ya safari za utalii na kutafuta wapenzi inayojaribu kutumia maeneo yetu ya kihistoria na turathi lazima isimamishwe mara moja na serikali ya Ethiopia ," Alisema afisa wa baraza hilo la Muungano wa madhehebu ya kidini Tagay Tadele, katika mazungumzo na shirika la habari la AFP. 

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinaweza kusababisha muhusika kufungwa kihfungo cha hadi miaka 15 jela kulingana na kipengele cha 629 cha sheria ya uhalifu ya Ethiopia. 

No comments

Powered by Blogger.