Waziri wa Ujenzi awasilisha Bungeni Bajeti ya Tsh. Trilioni 4.9


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amewasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Shilingi Trilioni 4.9. 

Katika fedha hizo shilingi Trilioni 1.3 ni kwa ajili ya Sekta ya Ujenzi, Shilingi Trilioni 3.6 ni kwa ajili ya sekta ya Uchukuzi na shilingi Bilioni 3.9 ni kwa ajili ya sekta ya Mawasiliano. 

Kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Wakala wa Barabara Tanzania umepanga kujenga barabara zenye urefu wa Km 432.30 kwa kiwango cha lami. 

Pia imepanga kujenga madaraja 13 pamoja na ukarabati wa Km 56 kwa kiwango cha lami katika barabara kuu.

Ili kuboresha utendaji wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwa mwaka wa fedha 2019/20 serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha malipo ya Ndege ya Pili aina ya Boeing 787 Dreamliner na ndege ya nne aina ya Bombadier Q400. 

Pia itafanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya aina ya A220-300, Ununuzi wa ndege moja aina ya Bombadier Q400 na injini ya akiba kwa ajili ya ndege aina ya Bombadier Q400

No comments

Powered by Blogger.