Muhongo na Ngeleja wakumbukwa na Kalemani


Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametambua mchango wa mawaziri waliomtangulia katika Wizara hiyo hususani katika uendelezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). 

Dk Kalemani ametoa kauli hiyo leo Mei 31 Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya TPDC. 

Amesema  shirika hilo limepata changamoto nyingi na watumishi mbalimbali wakiwamo mawaziri wameshiriki katika mafanikio yake. 

"Hii ni bahati kubwa sana, mimi nina miaka minne tu katika wizara hii( kama Waziri), sifa zote leo nazipata lakini wako watumishi waliotumikia miaka kumi, 20 na mawaziri wenzangu waliomtangulia akiwamo profesa Muhongo, Ngeleja na wengine wengi, " amesema Dk Kalemani.

No comments

Powered by Blogger.