Tatizo la kukosa choo

Tatizo la kukosa choo (constipation) ni tatizo ambalo limekuwa likiwakumba watu wengi  sana katika   dunia, watu wamekuwa wakiteseka bila kujua nini chanzo cha tatizo hili na vipi kuliondoa tatizo hili na wengine wamekuwa wakilipuuzia bila kujua madhara ambayo wanaweza kuyapata kutokana na tatizo hili. 

Tatizo hili hutokea pale mtu anakula vizuri lakini unakata siku tatu hadi nne bila kupata choo. Ukiona unakula kutwa mara tatu na unakaa siku mbili hadi tatu huendi chooni au unatoa choo kigumu kama mbuzi hilo ni tatizo kwako. 

Tafiti zinaonyesha mtu anaweza kupoteza maisha kama atakosa choo kwa siku tano hadi saba mfululizo.Watu wengi hulidharau tatizo hili lakini linamadhara makubwa tofauti na wanavyofikiria. 

Zifuatazo ndizo sababu za kukosa choo; 

Kupenda kula saana vyakula vilivyokobolewa (mfano ugali wa sembe,mikate n.k) 

Ukosefu wa mbogamboga za majani na matunda ya faiba kama machungwa,ukosefu wa kula mboga za majani na matunda hasa ya faiba kama machungwa huongeza tatizo hili.kila mtu anatakiwa kula matunda aina mbili na mboga za majani aina mbili kila siku. 

Matumizi makubwa ya pombe na sigara 
 Unywaji mdogo wa maji. Kila mtu anapaswa kunywa maji kwa kiwango cha chini lita 3 kila siku na usinywe maji wakati unakula, kunywa maji nusu saa kabla au baada ya kula. 

Matumizi mabaya ya madawa. Mfano dawa za presha, aleji n,k. 

Kuugua kisukari au ugonjwa wa misuli. 

Kansa ya utumbo mpana 

Yafuatayo ndiyo  madhara yatokanayo na kokosa choo; 

Unaweza kuugua saratani ya utumbo mpana. 
Unaweza kupata tatizo la tumbo kujaa gesi. 
Figo yako inaweza isifanye kazi vizuri. 
Unawezasababisha magonjwa ya moyo. 
Unaweza pata tatizo la kukakamaa mishipa ya damu ambapo utasababisha miguu kuwaka moto na ganzi miguuni au mikononi. 
Unawezasababisha magonjwa ya ini 
Unawezapata kisukari 

No comments

Powered by Blogger.