Okwi avipiga mkwara vilabu vya Ligi Kuu Bara
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi amevitahadharisha vilabu vya Ligi Kuu Bara kuwa hakuna atakayebaki salama mbele yao kwa kuhakikisha wanashinda mechi zao zote ili waweze kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Okwi alisema malengo yao ni kuhakikisha wanafanikiwa kutetea ubingwa wao kwa kushinda kila mchezo uliopo mbele yao ukiwemo wa leo.
“Sasa hivi tunaangalia mechi za mbele ikiwemo baada ya Azam, sisi hatuangalii zimebaki mechi ngapi, tunaangalia kushinda kila mechi baada ya nyingine kwa sababu tunachokitaka ni kupata pointi tatu.
“Kuifunga Yanga ni ushindi kama ulivyo ushindi wa kawaida, ndiyo ni derby lakini hilo lishapita na limebaki kwenye historia ila kwa kuwa tumemfunga, aliyekuwa juu yetu imeongeza kitu maana malengo ni kuchukua ubingwa,” alisema Okwi.
Simba ina pointi 45, wakizidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili baada ya kuicharaza leo mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment