Mambo ya msingi ya kuyaepeka katika safari yako ya mafanikio

Wakati mwingine yapo mambo ya msingi unayopaswa kuyaepeka ili uweze kufanikiwa kimaisha na mambo kama utaendelea kuyabeba basi kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo utakavyozidi kuwa maskini. 

Yafuatayo ndiyo mambo ya msingi ya kuyaepeka katika safari yako ya mafanikio: 
Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe 

Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake, na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote. 

Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako. 

Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya yaliyopita 
Kuhisi kwa kuwa kuna kitu Fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basi 

Maisha hayatawezekana tena. Pengine ulifiwa, kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au kufilisika. Matukio kama haya huwafanya watu wengi waishi maisha yasiyokuwa na furaha na mafanikio. 

Kukubali kuzungukwa na watu wasiokufaa 
Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali kushindwa, huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu nao watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa tayari kupiga hatua zaidi. Hivyo kama kweli unataka kupiga hatua za kimafanikio watu wa aina hii ni wa kuwakwepa. 

Kukimbia matatizo na kuogopa kushindwa 
Je wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila tunapoanguka. Na epuka Kuhisi kuna mtu mwingine anahusika na furaha yako. 

Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe 
Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu, kuiba, kuua nk! 

Kulaumu Vitu vinavyotokea na kutokuwa tayari kutafuta suluhisho Pengine kwa kutotaka kufanya maamuzi magumu au kutojua Majukumu yako ni yapi (badilika) 

No comments

Powered by Blogger.