Hamasa muhimu ya mafanikio ya mwaka mpya 2019

Mwaka mpya  umeanza rasmi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutupigania mpaka dakika hii. Naomba nikukaribishe rasmi hapa www.mrmoemedia.blogspot.com tuweze kujifunza  kwa pamoja mbinu mpya zitakazotusaidia kuweza kutimiza matakwa ya mafanikio tunayoyahitaji katika mwaka huu. 

Najua ya kwamba kiu ya kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa bado unayo ila naomba nikwambie ya kwamba  kama kweli unataka kupiga hatua za kimafanikio unatakiwa  pia kuhakikisha unabadili mbinu mbalimbali za kufanya mambo yako yote ya msingi yaletayo mafanikio. 

Nasisitiza juu ya suala hilo  kwa sababu  kama utaendelea kutumia mbinu zile zile ambazo ulizoea kuzitumia katika kutekeleza mambo yako mbalimbali ya kimafaniko basi jiandae kupata matokeo yale yale ambayo uliyoyapata mwaka jana. 

Hamasa ya mafanikio ya mwaka 2019 
Tambua kuwa huu ni mwaka mpya na wenye neema zake nyingi juu yako kama utaamua kuwa ni mtu chanya na mwenye kubadili mawazo yako kuwa vitendo halisi. Hakuana mwanadamu aliyeumbwa kuwa na maisha ya dhiki, bali ugumu wa maisha tumeutaka wenyewe kwa kuamua kuzikaza akili zetu. 

Tunatakiwa kubadililika kuanza sasa kwa kuamini kuwa sisi ni zaidi ya nyama na mifupa, sisi ni tofauti na ng'ombe, kwani tumepewa uwezo mkubwa sana wa kuweza kufanya mambo mbalimbali yaletayo mabadiliko makubwa katika dunia hii. 

Tunao uwezo wa kufanya mambo makubwa sana kama tukiamua kujitambua kuanzia sasa, Hatukuja duniani kushangaa yanayoendelea, bali tulikuja dunia kutimiza mambo yote ya kiutashi ambayo mwenyezi Mungu aliyaweka katika vichwa vyetu. 

Ndugu yangu acha kuwa mnyonge kwa kuiona dunia kama sio sehemu salama sana kwako, amini unao uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa pia. 

Ndugu yangu wa damu, hajalishi ni mambo mangapi amabayo umeyapitia, elewa na tambua  hayo yote yatokea kama sehemu ya vipimo vya uvumilivu wako katika kuhimili mikikimikiki ya kuelekea kule utakako. 

Acha mara moja  tabia ya kukutaa tamaa kwani kukutaaa tamaa ni dhambi pia ni chukizo mbele ya Mungu wetu Mwema, amua sasa, nyanyuka na uanze upya kupambana na mambo mbalimbali yatakayokusaidia kuweza kupiga hatua za kimafanikio. Kila siku jifunze kuifanya dunia hii iwe sehemu salama kwako. 

Jifunze kutofautisha kati ya mvua na jua, jifunze kutofautisha kati ya mjini na kijijini, jifunze kuishi na watu vizuri, jifunze kupenda na kusamehe, jifunze kuwa ni mtu chanya kila siku, jifunze kuchua hakua kwa kila fursa inayojitokea mbele yako, jifunze kupambanua kati ya pumba na mahindi, Jifunze kutafuta majibu sahihi  kwa kila changamoto inayojitokeza mbele yako. 

Mwisho naomba niweke nukta kwa kusema ya kwamba "Upya wa mwaka ni mabadiliko ya kalenda, hivyo unatakiwa kuanza kufanya mambo katika fikra na mtazamo tofauti na ulivyozoea hapo awali." 

Nikutakie siku njema na  Mafanikio mema, mwaka 2019 akawe ni mwaka wa mapambano dhidi ya umaskini. 

No comments

Powered by Blogger.