Alikiba atoa siri kwenye wimbo wake mpya



Msaniii wa muziki Bongo, Alikiba ameeleza maana ya 001 kwenye wimbo wake mpya wa 'Kadogo' neno ambalo amelitaja mwanzoni wa wimbo huo. 

AliKiba amesema 001 inawakilisha Mombasa ambapo ndio mke wake anatokea. 

"Inawakilisha Mombosa na huku ndipo alipotokea wife wa dunia na vile vile mshikaji wangu Hasssan Joh, Gavana na yeye alitusaidia vitu vingi sana na yeye ni mlezi wetu," alisema Alikiba kwenye mahojiano na The Playlist ya Times FM. 

Wimbo Kadogo unaendelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa una views zaidi ya milioni 2 kwenye mtandao wa YouTube.

No comments

Powered by Blogger.