Yanga yashindwa kutamba kwa Ndanda FC
Klabu ya Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 na 'Wanakuchele' Ndanda Fc katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na kusalia katika nafasi yake kwenye msimamo wa ligi.
Yanga walikuwa wa kwanza kufungwa na Ndanda kupitia Nassor Hashim mnamo dakika ya 16 tu ya mchezo.
Yanga nao walifanikiwa kujibu mapigo kwa kusawazisha kupitia mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajibu ambao ulimfika Japhary Mohammed na kuumalizia kwa njia ya kichwa ikiwa ni dakika ya 24.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 26 sawa na Simba ikiwa imecheza michezo 10.
Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 1-1 Ndanda FC.
Matokeo ya michezo mingine ni katika mchezo wa mapema zaidi uliozikutanisha Kagera Sugar dhidi ya Azam Fc, ambapo Azam Fc imeibuka na ushindi wa bao 1-0, bao pekee lililofungwa na mshambuliaji Donald Ngoma ambaye alipewa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha mchezo.
Mchezo uliochezwa saa 10:00 jioni, umeshuhudia Mwadui Fc ikitoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Post a Comment