Waziri Kairuki: Vituo vya umahiri kuchochea shughuli za uongezaji thamani madini



Imeelezwa kuwa, vituo vya Umahiri vinavyojegwa maeneo mbalimbali nchini vinatarajiwa kuwa kichocheo cha shughuli za uongezaji thamani madini nchini kwa kuwa, vinatarajia kutoa mafunzo ya uchimbaji bora wa madini ikiwemo uongezaji thamani madini, ukataji na ung’arishaji madini. 

Hayo yamebainishwa Novemba 20 na Waziri wa Madini Angellah Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Umahiri cha Musoma kinachojengwa na Mkandarasi kampuni ya SUMAJKT na kusimamiwa na kampuni ya Sky Architects. 

Katika ziara hiyo, Waziri Kairuki ameambatana na Naibu  Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini, Andrew Eriyo pamoja na Watendaji wa  Ofisi ya Madini Mkoa wa Mara na uongozi wa Mkoa wa Mara. 
nye tija. 

Pia, amesema serikali itaendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini kufanyika nchini ikiwemo kuhakikisha kwamba inajenga  maeneo mengi zaidi ya vituo hivyo. 

Vilevile, amezungumzia kituo cha mfano cha Lwamgasa kinachojengwa mkoani Geita, na kueleza kuwa, serikali inaangalia uwezekano wa kuwa na kituo kama hicho katika maeneo mengine na kuongeza, “tunaangalia sehemu nyingine baada ya kuwa na kituo cha mfano cha Lwamgasa huenda tukajenga kituo kama hicho hapa Musoma”. 

Kituo cha Lwamgasa ni moja ya vituo ambavyo vinalenga katika kutoa mafunzo kwa  vitendo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kuhusu uchimbaji wenye tija ikiwemo uchenjuaji bora pasipo kutumikia kemikali. 

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya tarehe 29 Oktoba,  kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wizara ilieleza kuwa kazi ya ujenzi wa mgodi wa Lwamgasa na usimikaji mitambo ya uchenjuaji katika kituo  hicho imekamilika kwa asilimia 80.

No comments

Powered by Blogger.