Watuhumiwa wa kifo cha shemeji yake Dj Khaled watiwa mbaroni

Idara ya Haki nchini Marekani ilitangaza kuwashikilia Watuhumiwa watano waliohusika na mauaji ya Josephat Tuck  ambaye ni shemeji yake Dj Khaled aliyeuwawa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kupigwa risasi. 

Ilielezwa kuwa mauaji hayo yalifanyika baada ya Tuck kupishana kauli kwenye ishu ya dawa za kulevya lakini baadae taarifa hizo zilikanushwa na kusema kuwa Josephat hakuenda nyumba sahihi na hivyo kujikuta akiingia nyumba ya wauza dawa za kulevya na hivyo kupigwa risasi. 

Idara ya haki nchini humo imeeleza kuwa mpaka sasa imewafungulia watuhumiwa hao mashtaka matatu ikiwemo ukabaji, wizi pamoja na mauaji huku ikiwa imetoa orodha kamili ya washtakiwa ambao ni Luis Semiday, Richard Jimenez, Kevin Cruz, Ira Lawson na Curtis Hines.

No comments

Powered by Blogger.