Utunzaji wa misitu na athari za uchomaji wake kwa jamii


Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. 

Aina za misitu 

Misitu inaweza kuwa ya asili au ya kupandwa na binadamu (isiyo ya asili).

Misitu ya asili ni misitu ambayo huota yenyewe bila kupandwa na mwanadamu. Kwa mfano, msitu wa Udzungwa (Mkoa wa Morogoro, Tanzania). 

Misitu isiyo ya asili ni misitu ambayo hupandwa na mwanadamu. Ndiyo tofauti kati ya misitu ya asili na isiyo ya asili. 

Umuhimu wa misitu 
Mara nyingi wanyama mbalimbali, wakubwa kwa wadogo, huishi na hutegemea uoto huo kwa kuwatimizia mahitaji yao ya malazi na chakula. 

Hata hivyo maisha ya binadamu hutegemea mazingira yake yanayomzunguka katika kujikimu kwani kupitia misitu mvua hunyesha na hivyo kusababisha ustawi na ongezeko la chakula. 

Ni kwamba asilimia kubwa ya watu hutegemea kilimo ili kujipatia mahitaji yao ya kila siku, hasa katika nchi za Afrika ambazo ziko nyuma sana katika nyanja za utumiaji wa teknolojia za kisasa kama utumiaji wa zana za kilimo, mf. matrekta. 

Hivyo katika kutimiza upatikanaji wa chakula kwa wingi ni lazima misitu ilindwe kwa nguvu zote katika ukuaji na ustawi wa jamii. 

Majukumu kuhusu misitu 

Tunatakiwa tutunze misitu kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe na vizazi vingine kwa sababu misitu inatusaidia kwa utalii na tunaweza kupata mvua. 

Njia za kufuata katika utunzaji wa misituː 
◾kupanda miti sehemu iliyokatwa miti 
◾kupunguza kilimo cha kuhamahama
◾kuzuia uwindaji wa wanyama kwa kuchoma misitu 
◾kuzuia ongezeko la watu katika eneo dogo 
◾kuelimisha jamii juu ya utunzaji misitu 

Faida za misitu ni: 
◾Husaidia katika mfumo wa mvua 
◾Hutumika kama makazi ya wanyama 
◾Ni chanzo cha mapato ya nchi 
◾Hutupatia dawa na chakula 
◾hutupatia mbao kwaajili ya ujenzi 

Hasara za ukataji mitiː 
◾unasababisha mmomonyoko wa udongo 
◾unasababisha ukame 
◾unakaribisha jangwa 
◾unasababisha mvua za misimu 
◾uharibifu wa mazingira 
◾ongezeko la hali joto 
◾uharibifu wa makazi ya wanyama. 

Hivyo ni bora kutunza misitu kwa ajili ya manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo. Ni muhimu kuwashauri watu watunze sana vyanzo vya asili kama misitu: hii ni kwa faida yetu wenyewe, inatusaidia hata kupata mvua kwa wingi.

No comments

Powered by Blogger.