Ubelgiji na fedha za Muammar al-Gaddafi

Huenda  fedha za Muammar al-Gaddafi zilizotaifaishwa Ubelgiji zimetumwa kwa makundi yanayofanya biashara haramu ya binadamu Libya. 

Kulingana na taarifa zilizotolewa na  kituo cha  habari cha RTBF cha nchini Ubelgiji zimefahamisha kuwa heunda fedha za aliekuwa rais wa zamani wa Libya Muammar al-Gaddafi zilizotaifishwa  katika benki za Ubelgiji yametumiwa makundi aambayo yanajihusisha na biashara haramu ya binadamu nchini Libya. 

Iwapo taarifa hizo zinathibitishwa itakuwa wazi kuwa  Ubelgiji imechugua upande wake wa kunnga mkono makundi ya wapiganaji  na biashara ya wahamiaji inayopigwa vita na ulimwengu mzima nchini Libya. 

Umoja wa Mtaifa umesema kuwa kwa lengo la kuzuia fedha za rais wa zamani wa Libya zisirejee katika mikono ya watu wasiostahili, baraza  la usalama la Umoja wa Mataifa  lilichukuwa uamuzi wa kutaifishwa kwa mali ni milki za Muammar al-Gaddafi katika benki nne nchini Ubeligiji : BNP Paribas Fortis (milioni 43), ING (milioni 376 ), KBC (milioni 869 ), Euroclear Bank  bilioni 12,8. 

Kituo hicho kimefahamisha kuwa pesa hizo  hazikutaifishwa. Mwaka 2012 kati ya bilioni 3 hadi 5 zilitolewa katika benki  za Ubelgiji ilifahmsihwa katika makala ilitolewa na kituo cha habari cha RTBF. 

Kituo  hicho kimemtaja waziri wa zamani wa fedha Didier Reynders ambae ni waziri wa mambo ya  nje aliruhusu fedha hizo kutolewa.

No comments

Powered by Blogger.