Mwadui FC waipiga mkwara Yanga
Uongozi wa Mwadui FC, umesema kuwa wataisimamisha timu ya Yanga katika uwanja wa Kambarage ili kuweza kuvunja rekodi ambayo haijavunjwa mpaka sasa katika michezo 10 waliyocheza timu ya Yanga.
Katika michezo 10 ambayo Yanga wamecheza hawajapoteza hata mmoja zaidi ya kutoa sare michezo 2 na kushinda michezo 8 na wamejikusanyia pointi 26 wakiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo.
Katibu wa Mwadui FC, Ramadhani Kilao amesema wanatambua ubora wa wapinzani wao ila hawana hofu kwa kuwa hesabu zao ni kuchukua pointi tatu.
"Hatutishwi na ubora wa kikosi cha wapinzani wetu, nasi pia tuna uwezo wa kuwasimamisha katika uwanja wetu wa Kambarage kwa kuwa wanaujua vizuri hivyo tumejipanga kuchukua pointi tatu nyumbani," alisema.
Mchezo wa Yanga na Mwadui utachezwa Novemba 22 katika uwanja wa Kambarage utakuwa ni wa kwanza kwa Yanga kucheza mkoani.

Post a Comment