Marekani yaitaka Saudia kufahamisha ulipo mwili wa Jamal khashoggi

Marekani yatolea wito Saudia kufahamisha ulipo mwili wa Jamal khashoggi  na kukabidhiwa familia yake kwa ajili ya mazishi. 

Wito huo umetolewa na Marekani kwa ajili ya kuandaliwa mazishi. 

Wito huo umetolewa katika tangazo lililosomwa na  naibu msemaji  katika ofisi ya rais  Robert Baladino Alkhamis usiku  katika mkutano na waandishi wa habari. 

Baladino amesema kuwa Marekani itaomba maelezo kufuatia kifo cha Jamal Khashoggi. 

Ifahamike kuwa mahakama ya mjini Istanbul alithibitisha kuwa Jamal Khashoggi aliuawa kwa kunyongwa na baade viungo vyake kukatwakatwa. 

Mwanahabari huyo alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai Oktoba 2 akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbl alipokuwa amejielekeza kwa ajili ya kufuatilia  hati zake za ndoa na Hatice Cengiz. 

Baada ya siku 18 Saudia ilikiri kuwa Khashoggi aliuawa katika ubalozi wake baada ya kukana. 

Baada ya uchunguzi  ulioendeshwa na jeshi la Polisi la Uturuki , Saudia ilifahamisha kuwa washukiwa 18 wamekamatwa nchini Saudia. 

Hapo awali Saudia ilifahamisha kuwa Khashoggi aliondoka katika  ubalozi huo, baada ya muda kubadili kauli na kusema kuwa alifariki  baada ya kuzuka ugomvi na maafisa katika ubalozi wa Saudia Istanbul.

No comments

Powered by Blogger.