Ijue Pumu ya Ngozi (eczema

Pumu ya Ngozi ni nini ? 

Pumu ya Ngozi ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha kuvimba kwa ngozi (inflammation). Hii huambatana na ngozi kuwasha, kuwa nyekundu, kavu, vipele na mabaka. 

Nini husababisha Pumu ya Ngozi ? 

Pumu ya ngozi husababishwa na mshituko wa kinga ya mwili (hypersensitivity) na ngozi ya mwili. Kuna uhusiano wa pumu ya ngozi na magonjwa kama asthma, mafua, msongo (stress) na kurithi (vinasaba). 

Dalili za Pumu ya Ngozi : 

Dalili kuu tatu wa Pumu ya Ngozi ni ngozi kuwa nyekundu, kuvimba na kupasuka. Pia huambatana na muwasho na kukauka kwa ngozi. 

Hii huambatana na magonjwa ya njia ya hewa kama asthma (atopic dermatitis) au baada ya kukutana na kitu kinachosababisha mshituko wa kinga ya mwili na ngozi mfano kipodozi au kemikali nk (contact dermatitis). 

Pumu ya ngozi kwa watoto : 

Asilimia 8 mpaka 18 ya watoto wote uhathiriwa na ugonjwa huu. Hii huambatana na mabadiliko ya hewa na magonjwa ya mfumo wa hewa mfano mafua na asthma. Mara nyingi ugonjwa huu hupotea ukubwani baada ya matibabu. 

Tiba ya Pumu ya ngozi: 

-Tiba kuu ya ugonjwa wa pumu ya ngozi ni kuondoa ukavu kwa kuiweka ngozi na unyevu nyevu. Madaktari hushauri kutumia mafuta ya Vaseline yasiyo na manukato. Pia mgonjwa hushauriwa kuogea sabuni isiyo na manukato mfano sabuni ya kipande B-29. 

-Daktari pia anaweza kutoa dawa ya kupunguza uvimbe (antiiflammation drug) ya kupaka kama ataona inafaa. 

-Daktari pia anaweza kutoa dawa ya kuzuia kinga ya mwili isishambulie ngozi (immunosuppresors drugs). 

-Mgonjwa hushauriwa kuchunguza vitu au dawa zinazosababisha ugonjwa huu na kuviepuka mfano aina za vipodozi na kadhalika. 

Inashauriwa kupata ushauri wa daktari kila unapopata dalili za ugonjwa wa ngozi. 

No comments

Powered by Blogger.