Cuba yaendelea kuadhibiwa na Marekani

Kuhusiana na vikwazo vya kibiashara na uchumi ambavyo Marekani imeiwekea serikali ya Cuba, kwa mara nyingine katika kura iliyopigwa na wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuiondolea vikwazo  vya kiuchumi Cuba , Ingawa nchi 187 zimeunga mkono, Marekani na Israel zimepinga pendekezo hilo na hivyo basi kuendelea kuiadhibu Cuba. 

Marekani kwa mara nyingine tena imepiga kura ya kupinga kuiondolea vikwazo vya kiuchumi Cuba, tangu mwaka 1992 umoja wa mataifa umekuwa ukipendekeza vikwazo hivyo viondolewe lakini Marekani imekuwa ikipinga. 

Hii ni mara ya 27 umoja wa mataifa kuleta pendekezo hulo la Marekani  isitishe   vikwazo hivi vya kiuchumi na kibiashara dhidi ya Cuba. 
Kati ya nchi 193 zilizopiga kura kwenye pendekezo hilo, nchi 189 ziliunga mkono vikwazo hivyo dhidi ya Cuba viondolewe. 

Marekani kama inavyofanya kila mwaka ilipinga tena pendekezo hilo, Izrael nayo ilipinga huku Ukrain na Moldovia hawakupiga kura. 

Wajumbe wakudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa Urusi na China zilipiga kura kuiunga mkono Cuba kwamba vikwazo hivyo viondolewe. 

Uhusiano baina ya Cuba na Marekani ulionekana kama unaanza kurudi katika hali ya kawaida mwaka 2015, wakati nchi hizo mbili zilipofanya mazungumzo kufikia Marekani kufungua ubalozi Havana, na Cuba kufungua ubalozi Washington.Mwaka 2016  kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992 Marekani haikupiga kura. 

Uongozi wa rais Trump  tangu uingie madarakani uliamua kuendelea na vikwazo hivyo dhidi ya Cuba. 

Maamuzi ya umoja wa mataifa sio lazima kuyafuata ila ni ushauri na yanaonyesha msimamo wa jamii ya kimataifa. 

 Marekani iliiwekea Cuba vikwazo kwa mara ya kwanza mwaka 1960, kadiri miaka inavyopita wamekuwa wakiongeza vikwazo hivyo.

No comments

Powered by Blogger.