BMT yaijia juu Yanga

Baraza la Michezo nchini (BMT), limeitaka Yanga kufanya uchaguzi na usimamiwe na TFF kutokana na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo kutojitosheleza hivyo inahitaji usimamizi wa shirikisho. 

Kwa mujibu wa taarifa ya BMT iliyotolewa leo ni kwamba baraza hilo limepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanachama juu ya mapungufu ya uongozi wa Yanga katika baadhi ya nafasi hiyo kuamuru uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo. 

Aidha BMT imeagiza wanachama wote ambao hawana kadi kwenda kwenye matawi yao kujisajili na kupata kadi ndani ya wiki tatu kuanzia sasa. 

Vilevile BMT imelitaka Shirikisho la Soka nchini(TFF) kuchagua tarehe ya uchaguzi na itangazwe mwezi huu. Nafasi zitakazojazwa katika uchaguzi huo ni pamoja na ya Mwenyekiti iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Manji. 


No comments

Powered by Blogger.