Tunawafahamu waliomuua Khashoggi, muili wake upo wapi"- Erdoğan

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa   aliemuua Jamal anatambulika ila bado kumfahamu alietoa amri ya kuuawa mwanahabari huyo. 

Rais Erdoğan amesema kuwa Saudia ilitakiwa kuwataja waliotekeleza mauaji ya Jamal Khashoggi. 

Katika mkutano na viongozi  kata wa chama cha AK, rais Erdoğan amesema kuwa  mauaji ya Jamal Khashoggi ni  jambo la kukemea. 

Jamal Khashoggi alionekana kwa mara ya mwisho akiwa hai Oktoba  2 akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul. 

Jamal Khashoggi alijielekeza  katika ubalozi mdogo wa Saudia kwa ajili ya kamilisha masharti ya ndoa yake . Aliingia katika ofisi za ubalozi huo  na kutoeka moja kwa moja. 

Rais Erdoğan amesema kuwa baada ya uchunguzi  imefahamishwa kuwa Khashoggi aliuawa katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul. 

Madai ya Saudia hapo awali kuwa Khashoggi aliondoka katika ubalozi  ni jambo la kushangaza na lenye mashaka aliendelea kusema rais Erdoğan. 

Kusema kuwa Jamal alitoka katika ubalozi huku mchumba wake asiende kumtafuta ni jambo la kustaajibsha na kauli hiyo ni kauli ya kitoto ambayo haistahili kutamkwa na kiongozi wa taifa kubwa. 

 Rais Erdoğan ameghadhibishwa na tukio hilo na kusema kwamba tunatambua kuwa Khashoggi ameuawa, muili wake upo wapi ameuliza rais wa Uturuki. 

Rais Erdoğan ameendelea kuhoji kuhusu kukamatwa kwa watu 18 Saudia  na kusema kuwa watu hao wanamtambua vema alieendesha mauaji ni nani alietoa amri. 

Ni nani ametoa amri kwa watu hao  kuja Uturuki ameuliza rais Erdoğan.

No comments

Powered by Blogger.