Rais wa Interpol asakwa, China yatakiwa kueleza aliko
Shirika hilo linasema kuwa lina wasiwasi kuhusu hali ya sasa ya Rais wake.
Familia haijawasiliana naye tangu andoke makao makuu ya Interpol nchini Ufaransa mjini Lyon tarehe 25 Septemba. China haijasema lolote.
Gazeti la South China Morning Post lilikunuu taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.
Haijulikani ni kwani nini alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu au alikuwa anazuiliwa
Mapema wiki hii mwanafilamu Fan Bingbin, ambaye alitoweka nchini China, aliibuka akiomba msamaha na faini ya dola milioni 129 kwa kukwepa kulipa kodi na makosa mengine.
Alichaguliwa rais wa Interpol mwezi Novemba mwaka 2016, raia wa kwanza wa China kuchukua wadhifa huo na anatarajiwa kuwa katika wadhifa huo hadi mwaka 2020.
Yeye ni mkuu wa kamati kuu cha shirika hilo ambalo hutoa mwongozo mzima wa Interpol.
Kabla ya kuchukua wadhifa huo, Bw Meng alikuwa naibu waziri wa masuala ya usalama wa umma nchini China na bado yeye ni mwanachama wa cheo cha juu wa chama cha Communist.
Pia ana ujuzi wa miaka 40 ya ujuzi wa sheria ya uhalifiu nchini China hasa katika nyanja za madawa ya kulevya, ugaidi na udhibiti wa mipaka.
Baada ya kuchaguliwa kwake makundi ya haki za binadamu yalielezea wasi wasi kuwa hatua hiyo itaisadia China kuwatafuta watoro wa siasa ambao waliikimbia nchi.

Post a Comment