IGP Sirro - Swala la dhamana halina mjadala, atoa agizo kwa askari wote nchini



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro ametilia mkazo suala la utolewaji wa dhamana kwa watuhumiwa wenye makosa yanayokubaliwa dhamana na kukidhi vigezo pasipo kuzingatia siku na muda wa kutolewa kwa haki hiyo. 

IGP Sirro amezungumzia jambo hilo akiwa Jijini Arusha akitokea mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa shughuli za kila siku za Jeshi hilo. 

Sirro amewataka askari wake kwenye maeneo yote nchini kufuata weledi na kwamba suala la dhamana kwa watuhumiwa wanaokidhi vigezo halina mjadala

No comments

Powered by Blogger.