Polisi wamnasa mtu anayehusishwa kutuma mabomu kwa wanasiasa
Maafisa wa polisi nchini Marekani wamemkamata mtu mmoja katika jimbo la Florida anayehusishwa na kitendo cha kutuma mabomu kwa wanasiasa kadhaa wa chama cha Democratic pamoja na wakosoaji wa Rais wa Marekani Donald Trump.
Maafisa wa polisi wamesema mshukiwa huyo ni mwanamume mwenye umri wa miaka 56 na mwenye rekodi ya kuhusika na vitendo kadhaa vya kihalifu ambae pia anadaiwa kuwa ni mfuasi wa Rais Trump ambaye amewahi kuhudhuria mikutano yake ya hadhara.
Hadi sasa polisi wameweza kuvipata vifurushi 13 vya mabomu vinavyotumwa kwa njia ya posta, na wametoa tahadhari kwamba huenda kukawepo vifurushi vingine zaidi ambavyo bado havikuweza kupatikana.
Vifurushi hivyo vya mabomu vimetumwa kwa watu kadhaa mashuhuri, ikiwa ni pamoja na Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na Hillary Clinton ambaye alikuwa mpinzani wa Trump katika uchaguzi wa Urais wa mwaka 2016.
Post a Comment