Mkude ampa tano kocha wa Yanga
Kiungo mkabaji wa timu ya Simba Jonas Mkude amempa tano kocha wa timu ya Yanga ,Mwinyi Zahera kumbadilisha Ibrahim Ajibu na kumtaka asibweteke kwa mafanikio aliyoyapata.
Mkude alisema kuwa juhudi za Zahera ndiyo zimemfanya Ajibu kuwa katika kiwango ambacho kimemwezesha kuongoza kupiga pasi za mabao nchini akiwa amepiga pasi 8 na kufunga mabao 3.
"Kusema kweli bila Zahera,naamini Ajibu asingekuwa tishio hivi sasa katika michuano ya ligi kuu,nasema hivyo kwa sababu sisi wachezaji tunajuana na huwa tunazungumza tunapokutana.
"Kila wakati huwa napata taarifa kuhusiana na Zahera jinsi anavyopambana na Ajibu ili kuhakikisha anakuwa fiti,na hiyo ni kwa sababu ameshamjua rafiki yangu huyo jinsi alivyo,hivyo namuomba Ajibu aendelee kuwa makini"alisema.

Post a Comment