Mafuriko yasababisha maafa makubwa

Watu zaidi ya 357,000 wameathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria. 

Kiongozi wa shirika la hali za dharura, NEMA, akiongea katika mji mkuu wa jimbo hilo, Yola alisema mafuriko yaliyotokanana na mvua kubwa kunyesha yameharibu nyumba zaidi ya 7893 na yameathiri watu zaidi ya 357300. 

Suleyman amesema wameomba msaada kutoka kwa serikali kuu na serikali za majimbo mengine kusaidia maeneo yalioathirika. 

Mafuriko yaliyotokea kipindi hiki cha masika nchini Nigeria yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200. 

No comments

Powered by Blogger.