DC awataka wananchi kuiunga mkono Serikali, ahimiza maadili mema
Waumini wakiislamu Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kusimama katika imani zao na kuwelekeza watoto wao mambo mema yanayo mpendeza mwenyezi Mungu ili Taifa lisipungukiwe wasomi kwa kukosa wataalamu kisa watoto wameshindwa kuendelea na masomo kwa kujiingiza katika mambo yasiyo faa ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.
Mjema ameyasema hayo katika maulidi ya Mtume Muhamad(S.A.W) na sherehe ya kutimzia miaka tisa ya kuanzishwa kwa Madrasa iliyo kinondoni ,na kuongeza kuwa kunafaida kubwa kuwalea watoto katika misingi ya dini kwani yatamsaidia mtoto na Taifa kupata wafanyakazi na raia wema.
‘’Tumekuwa na watu hawana maadili wanawalaghai na kuwa hadaa watoto wakiKe na wakiume nakuwaingiza katika matumizi ya dawaza kulevya wazazi tunakazi kulisimamia hili ‘’alisema
Aidaha amewataka kuitunza amani ya nchi na kuiunga mkono serika kwa kufanya kazi na kudumisha amani na kuwa na mshikamano , na kusema kuwa Serikali kali imeendelea kutoa mikopo nafuu kwa wananchi hasa vijana na akinamama waweze kuendeleza bishara na kujikwamua kiuchumi.
“Nnyiye akinamama wa wa kinondoni msikubali kukaka bila kazi serikali imekupeni fura kopeni mfanye biasha mikopo haina riba mytawezeshwa kuchimba madini kilimo , na sisi hapa pwani tunayo Bahari kopeni zana za uvuvi “ alisema.
Hata hivyo amewausia wasicha na kujitunza wasikatishe masomo kwaq kudanywa kwa taamaa ya vitu na kuwatia moyo kuwa wanaweza wasikate taamaa kwani wananwake wengi wamefanikiwa kuwa na elimu kubwa na kushika nyadhifa kubwa kitaifa .
“Tanzania ya viwanda inahitaji wasomi someni ili mlisaidie taifa msiige mabo ya hovyo katika mitandao tuchague mema na tuwe waamifu kwa jamii Mola wetu anatuusi mema”alisema
Pamoja na hayo Mjema amechangia jumla ya shilingi 50,000 kwa chuo hicho kwaajili ya kununulia mahema na viti vitakavyo saidi katika kuendeleza miradi ya kikundi hicho.
Madrasa hiyo ya akinamama ilianzishwa na Mufti wa Tanzani Shekh Abbubakari Zubery bin ALLY baada ya akina mama wa Kinondoni kumuomba baada ya wanafunzi kuongezeka ambapo ilianza na wana funzi 72 na sasa inawanafunzi wakium 119 na wakike 72.

Post a Comment