Baada ya Kipindupindu na Njaa sasa ni ugonjwa wa Dondakoo unaouwa zaidi watoto nchini Yemen
Katika hospitali ya umma iliyopo makao makuu ya Yemen, mjini Sanaa, madaktari wapo katika hali ya dharura baada ya mlipuko wa ghafla wa ugonjwa hatari wa dondakoo (diphtheria).
Wodi za wagonjwa wa mahututi zimejaa watoto na wanawake wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo, Ugonjwa huu unaosababishwa na aina fulani ya bakteria huenezwa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine kwa njia ya hewa, pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya.
Ugonjwa husababisha koo kuzibwa kwa aina flani ya tabaka nene, katika kesi ambazo ni mbaya ugonjwa huu humuua mtoto ndani ya masaa kama hajapata tiba.

Post a Comment