Zijue Faida Na madhara ya Matumizi Ya Chumvi Kifua


Bila shaka kila mmoja wetu anapenda sana kuitumia chumvi, na hii hutokea hasa pale anapokula chakula chenye uhitaji wa chumvi. Lakini Watu wengi wamekua wakiitumia chumvi kulingana na matakwa yao binafsi bila kujua bila kujua chumvi ina mahusiano yapi afya zao. Wengi hutumia kwa ajili ya kupata radha katika chakula anachokula. 

Wengi wetu wanakula chumvi bila hata kujua kiwango gani cha chumvi hitachohitajika mwilini? Je wewe ni miongoni mwa watu hao? Kama jibu ni ndio nakusihi ufutane na Dr. Julius Kimaro katika Makala haya kwani ameeleza kwa kina zaidi. Ambapo Anasema: 

CHUMVI 
Kikemia chumvi ina madini ya sodium chloride ambayo huitajika sana mwilini. Na madini hayo husaidia kwa kiwango kikubwa katika mwili wa mwanadamu kama ambavyo nitaeleza hapo chini: 

Faida za chumvi 
Moja kati ya faida kubwa ya chumvi ni kuweka sawa kiwango cha maji mwilini (fluid balance) kinachoptaikana katika mwili wa mwanadamu. 

Chumvi husaidia katika kuweka sawa mtiririko wa mapigo ya moyo (heart rhythm) pale inapotumika kwa usahihi.

Husaidia katika kutanuka na kusinyaa kwa misuli (contract and relax of muscles), ambapo misuli hiyo husaidia kwa kiwango kikubwa usafishaji wa damu na maji endapo itakuwa haijaithiriwa na kiwango cha chumvi kwa wingi. 

Madhara ya chumvi. 
Madhara makubwa yatokanayo na ulaji mbaya wa chumvi ni shinikizo la damu (blood pressure). Kwani ukweli usiopingika ni kwamba kuna mahusiano ya moja kwa moja ya utumiaji wa chumvi kwa wingi na na kupanda kwa presha. 

Hata hivyo wataalamu wa afya wamebaini ya kwamba uwepo sodium ambayo ipo kwenye chumvi ndiyo  chanzo kikubwa cha kuasababisha ugonjwa huo. Kwani tafiti zinaonesha ya kwamba binadamu akitumia chumvi kwa asilimia 40 ya uzito wake ana uwezo wa kupunguza kupata shinikizo la damu. 

Nini kifanyike: 
Muhumu kuzingatia kuwa kiwango salama cha chumvi kwa mtu mzima hutakiwa kula chumvi kiasi cha 500 milligram ambayo ni sawa na robo ya kijiko cha chai kwa siku ili kuweza kuepukana na matatizo yatokanayo na ulaji wa chumvi kwa wingi. 

Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema, na usisiahau kumshirisha na mwingine ujumbe huu, ili kulinda kizazi hiki kwa kuepeka matumizi mabaya ya chumvi. 

No comments

Powered by Blogger.