Kamati ya Bunge yahoji DAWASCO kufuta deni bilioni 24
Kamati ya bunge kilimo, mifugo na maji imehoji sababu ya wizara ya maji na umwagiliaji kushindwa kutoa taarifa, kuhusu shirika la majisafi na majitaka mkoa wa Dar es salaam (DAWASCO) kufuta deni la bilioni 24.4.
Kamati hiyo imedai deni hilo limefutwa bila kushirikisha mamlaka ya majisafi na majitaka (DAWASA), kama ilivyobainishwa katika ya ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2016/2017.
Hayo yamesemawa leo Mei 07 2018, na mwenyekiti wa kamati ya kilimo, mifugo na maji Mh.mahmoud Mgimwa wakati wa kuwasilisha bajeti ya kamati bungeni na kuongeza kumekuwepo kwa matumizi yasiyoridhisha ya shilingi bilioni 1.8 katika uunganishaji wa wateja wapya wa maji.
Kamati pia imedai DAWASCO imeshindwa kununua kifaa cha utambuzi wa uvunaji wa maji ambapo imepelekea upotevu wa maji zaidi ya 47%
Mwenyekiti Mgimwa amehoji ukosefu wa taarifa za madeni ya DAWASCO na DAWASA, pia hakuna taarifa za maslahi ya wafanyakazi, utaratibu wa ajira na taarifa za upotevu wa maji.
Awali wizara ya maji na umwagiliaji kupitia waziri wake Eng.Isack kamwele iliomba bunge kuizinisha kiasi cha shilingi bilioni 697.5 ambapo matunizi ya maendeleo ni bilioni 727.3.
Post a Comment