Brand ya African Boy imemfanya Jux kupata dili nono
Staa wa muziki wa RnB Juma Jux ambaye pia ni mpenzi wa muimbaji Vanessa Mdeeametuonyesha goodnews kupitia instagram account yake baada ya ku-sign mkataba na kampuni kubwa nchini China ya Chinese Manufacturer Vendom kwa ajili ya kuanza kufanya uzalisha wa bidhaa za brand ya African Boy.
Juma Jux alianzisha bidhaa za brand yake ya African Boy akiwa China kwa ajili ya masomo yake lakini kutokana na Wachina kushindwa kumuita jina lake walianza kumuita African Boy ndipo brand ya African Boy ilipoanza kukua na kujulikana hadi kuanza kutengeneza bidhaa mbalimbali.
>>>“Ilianza hashtag ya African Boy nikiwa kijana niliosoma na kuishi na kujituma nikiwa China, brand ilikuja kuwa mimi na mimi kuwa brand kutoka kwenye t-shirts, kofia mpaka viatu. Leo nina sign dili na Chinese Manufacturer Vendome, hii isingewezekana bila nyinyi , mmeifanya African Boy ya kwenu na mmeifanya ijulikane ulimwenguni”
Post a Comment