Beyoncé afanya kufuru kwenye tamasha la Coachella


Baada ya mwaka jana msanii wa muziki nchini Marekani, Beyonce kushindwa kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la muziki nchini humo la Coachella kutokana na ujauzito aliokuwa nao kipindi hicho, Hatimaye mrembo huyo asubuhi ya leo amefanya show ya historia kwenye jukwaa la tamasha hilo. 

Beyonce ambaye alipanda na wasanii wenzake wa kundi la Destiny’s Child Michelle Williams na Kelly Rowland walitumbuiza nyimbo zao kama  Say my name na Bills, Bills, Bills. Nyimbo ambazo ziliibua shangwe na baadaye Beyonce kuanza kutumbuiza na madensa wake. 

Beyonce hajawakuna mashabiki pekee bali hata wasanii wengine wakubwa nchini humo kama Chance The Rapper naye amempigia saluti Beyonce kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa show kali aliyofanya. 

Hata hivyo, huenda sasa hivi stori zingekuwa nyingine kama kama rapa pekee aliyechaguliwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo maarufu zaidi Marekani, Wizkid angefanikiwa kupanda jukwaani. 

Waandaaji wa tamasha hilo jana walitoa taarifa kuwa rapa huyo amekwama kuingia nchini Marekani na kuahidi mashabiki wa Tamasha hilo kuwa atatumbuiza wikiendi ijayo. 

Tamasha la Coachela linafanyika Indio, California na limeanza Ijumaa ya tarehe 13 Aprili na litamalizika Jumapili ya tarehe 15 Aprili 2018, Na limehudhuriwa na zaidi ya wasanii 120 wa muziki wa kimataifa

No comments

Powered by Blogger.