Ndege ya abiria 18 yaanguka DR Congo

Ndege ya abiria iliyokuwa ikiwabeba watu 16 imeanguka katika mji wa Goma mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya DR Congo.

Gavana wa jimbo la Kivu kaskazini Nzanzu Kasivita Carly amesema kwamba watu wamefariki lakini hakutoa idadi kamili .

Ndege hiyo ilianguka juu ya nyumba katika eneo jirani la Mapendo baada ya kushindwa kupaa katika uwanja wa ndege wa mji huo , aliongezea.

Ndege hiyo aina ya Doenier 228 ilikuwa ikimilikiwa na kampuni binafsi ya Busy Bee.

Ilitarajiwa kuelekea Beni yapata kilomita 350 kutoka kaskazini mwa Goma, wakati ilipoanguka dakika moja baada ya kupaa kulingana na chanzo kimoja katika mji wa Goma kilichozungumza na BBC.

Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini DR Congo , kutokana na viwango vya chini vya usalama na kutorekebishwa kwa ndege hizo.

Ndege zote za kibiashara za taifa hilo zimepigwa marufuku kufanya biashara katika Muungano wa Ulaya.

No comments

Powered by Blogger.