Kenya: Gari lililozama Likoni feri limetolewa
Gari lililozama baharini siku 13 zilizopita katika kivuko cha Likoni feri, mjini Mombasa pwani ya Kenya hatimae limetolewa.
Hii ni baada ya wapiga mbizi wa jeshi la Kenya kwa ushirikiano na wapiga mbizi kutoka Afrika kusini kufanikiwa kufikia gari hilo.
Miili ya mama Mariam Kighenda, 35, na mwanawe wa kike Amanda Mutheu, 4, pia imeopolewa kutoka ndani ya maji.
Aliyekuwa mume wa Marium, bwana John Wambua aliweza kutambua miili ya marehemu kabla haijaondolewa katika eneo la tukio.
Vilevile ibada maalum ya kuwaombea marehemu , iliendeshwa na mchungaji mara tu baada ya miili hiyo kutolewa kwenye maji.
Jitihada za kuopoa miili ya mama na mtoto wake wa kike waliokuwemo ndani ya gari hilo lililozama zilianza mnamo Septemba 29.
Wakenya wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao.
Wanamaji wa Kenya walipata shinikizo kubwa la kumaliza zoezi hilo la uopoaji kabla ya Oktoba 10 - tarehe inayoadhimishwa kama sikukuu ya Mashujaa iliyopangiwa kufanyika kitaifa katika mji huo wa Pwani ya Kenya.
Wakaazi walikuwa wametishia kuisusia sherehe hiyo ambayo rais Uhuru Kenyatta alitarajiwa kuhudhuria, iwapo miili hiyo haitakuwa imeopolewa.

Post a Comment