Ujue mchango wa marafiki katika kuyabadili maisha yako

Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.  Aina ya kwanza ni marafiki ambao ni wema na aina ya pili ni marafiki wabaya.

Tukianza na kuangalia aina hiyo ya kwanza, marafiki wema hao ni marafiki ambao ni watu ambao wana mawazo chanya katika kukushauri hata kutenda mambo mbalimbal yenye mchango mkubwa wa kuyabadili maisha yako kwa kiwango cha juu sana. Pia katika kundi hili la marafiki wapo marafiki wa aina hii wachache sana.

 Aina ya pili,marafiki wabaya hawa ni  marafiki ambao ni watu ambao hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa tu.

Watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu ambazo hatustili kuishi na watu hao .

Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba ushauri kwa watu ambao siyo sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao.

Tumekuwa tukushuhudia  baadhi ya wanafunzi ambao pindi waendapo  masomoni baada ya kufika huko wamekuwa na tabia za ajabu hii ni kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi.

Tumeona baadhi ya vijana hao wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,  utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.

Mpenzi msomaji wa makala haya naendelea tena juu ya somo hii la marafiki. Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo mazuri na kuwashirikisha marafiki zao, na marafiki hao wamekuwa wanazidi kuwakatisha tamaa tu.

 Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako na kumwambia nataka kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki uliyenaye utamsikia akisema Biashara hiyo hatatoka kwa sabubu fulani anaifanya au fulani kaliteka soko la biahara hiyo, hivyo hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya. Ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye.

Wapo baadhi ya marafiki ambo wao ukiwashirikisha jambo lako na wao huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata kidogo.

Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki sahihi ambao unahisi wewe wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke wanasema ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua marafiki wema. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.

Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia "always forward, backward never" ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko. Marafiki sahihi wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi kwa kile ulichowashirikisha na sababu za msingi.

Swali dogo la kujiuliza marafiki ulio nao ni wema au wabaya? kama ni wabaya unachukua jukumu gani baada ya kukupa somo hili?  ni muda wako mzuri wa kufikiri juu ya jambo hili na kuchukua uamuzi sahihi.

Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung'unike kutokana na magumu unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana mbele ya jamii.

No comments

Powered by Blogger.