Watu watatu wafungwa maisha jela kwa kumbaka msichana wa miaka 8
Mahakama moja nchini India leo imewahukumu adhabu ya kifungo cha maisha jela wanaume watatu waliotiwa hatiani kwa kumbaka na kisha kumuua msichana wa miaka minane katika jimbo la Jammu Kashmir.
Wakili wa upande wa utetezi, Farooqui Khan, amesema watu wengine watatu ambao wote ni maafisa wa polisi wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kuvuruga ushahidi.
Mwili wenye majereha wa msichana huyo kutoka jamii ya Waislamu wanaohamahama ulipatikana kwenye msitu karibu na mji wa Kathua mnamo Januari 2018.
Wanaume hao walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani ni Sanjhi Ram, afisa mstaafu wa serikali, afisa wa polisi Deepak Khajuria pamoja na Parvesh Kumar.
Watatu hao wamepatikana na hatia ya kubaka, kuua na matendo ya unyanyasaji miongoni mwa mashitaka mengine lakini wakili wao amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.
Post a Comment