Simba SC wajibu baada ya Yanga SC kutangazwa kucheza klabu Bingwa Afrika 2019/20


Baada ya shirikisho la soka Tanazania (TFF), kuthibitisha kuwa Tanzania imepewa ruhusa ya kuingiza timu nne kwenye michuano ya vilabu Afrika, klabu ya Simba imetoa ujumbe. 

Simba wameweka ujumbe kwenye mtandao wa Instagram, ikionesha kumbukumbu ya siku walipoitoa AS Vita na kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

''Ilikuwa siku ya kihistoria kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuongeza alama ambazo zimeiwezesha nchi yetu kuingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa msimu wa 2019/2020'' taarifa hiyo imeeleza. 

Kwa mujibu wa TFF, ni kwamba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limewathibitishia kuwa pointi ambazo zimepatikana katika miaka mitano iliyopita zimesaidia nchi kuongezewa timu mbili hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa zitakwenda Simba SC na Yanga SC huku shirikisho zikienda Azam FC na KMC. 

No comments

Powered by Blogger.