Ronaldo ampeleka Matthijs de Ligt Juventus

 Beki wa Ajax na timu ya Taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt amesema kuwa ameombwa kujiunga na mabingwa wa Italia Juventus na Cristiano Ronaldo wakati walipokutana kwenye mchezo wa fainali (Nations League final) siku ya Jumapili. 

Katika mchezo huo Ureno waliweza kunyakua ubingwa huo baada ya kuifunga Uholanzi bao 1-0 na baada ya mechi picha za tv zilimuonyesha Ronaldo akiwasiliana na Matthijs de Ligt. 

Ligt amethibitisha kuwa uwezekano wa kuhamia kwa mabingwa hao wa Italia unachochewa na mchezaji huyo mshindi wa Ballon d'Or kwa mara tano. 


No comments

Powered by Blogger.