Hii ndio misemo itakayokupa motisha ya kufanikiwa zaidi


Mafanikio ya maana tofauti kati ya mtu na mtu. Wengine wanaamini kwamba watakuwa wmefanikiwa wakiweza kuwa na pesa ya kiasi fulani. Ila kwa wengine, kuishi vizuri na kusaidia watu kupitia kazi yao ndio kufanikiwa.  Kama tulivvyo sema mwanzoni, maana ya kufanikiwa inatofautiana kati mtu na mtu. Ila, watu wenye mafanikio huwa wana sifa zinazofanana. 

Miongoni mwa sifa zinazofanana kwa watu waliofanikiwa ni pamoja na kujituma. Mtu aliyefanikiwa ni mtu anayeongea kwa matendo na sio maneno. 

Ila, kwa kuwa inaweza ikachukua muda kuwa na sifa zote hizo, tumia misemo 10 ifuatayo kukuongezea motisha: 

1. “Nafasi za kufanikiwa hazijitokezi hivi hivi, inabidi uzitengeneze” – Chris Grosser 

2. “Njia pekee ya kufanya kazi nzuri ni kupenda kazi yako. Kama hujapata kazi unayoipenda, endelea kuitafuta. Usiridhike” – Steve Jobs 

3. “Mtu asiyewahi kukosea hajawahi kujaribu kitu kipya” – Albert Einstein 

4. “Kama kila kitu kingekuwa kimekamilika, usinge jifunza chochote na usingekuwa” – Beyonce Knowles 

5. “Ndoto ni kitu nzuri. Ila, ni ndoto tu. Ndoto hazifanikiwa kuwa kweli kwa kuwa umeziota. Kuchapa kazi ndio inafanya ufanikiwe. Kuchapa kazi ndio kinachosabibisha mabadiliko” – Shonda Rhimes 

6. “Labda hautashindwa kama mimi nilivyoshindwa, ila, mara nyingine kushindwa hakuepukiki. Haiwezekani kuishi bila kushindwa kufanya kitu mara moja, labda uwe unaishi kwa tahadhari kwa kiasi kikubwa kwamba bora usingeishi kabisa – na hapo, tayari utakuwa umeshindwa” – J.K Rowling 

7. “Simjui mtu yoyote aliyewahi kufika ngazi za juu bila kuchapa kazi. Hiyo ndiyo kichocheo. Na labda haitakufikisha juu kabisa, ila utakaribia” – Margaret Thatcher 

8. “Kufanikiwa kwa kishindo, inabidi ujaribu kufanya vitu vikubwa” – Bill Gates 

9. “Bora uwe na marafiki waliokuzidi. Chagua marafiki wenye tabia nzuri kuliko ya kwako na utaishia kuwafuata” – Warren Buffet 

10. “Tunaweza tukashindwa mara nyingi, ila tusikubali kushindwa kabisa kabisa” – Maya Angelou 

Misemo yote haya yana ujumbe zinazofanana. Tegemea kushindwa, chapa kazi, chagua kazi unayoipenda na jihusishe na watu watakao kuongezea  motisha na kukusukuma ili ufanikiwe. 

Wote hawa walikuwa na mapambano yao binafsi ila hawakuruhusu kushindwa mara kwa mara iwakatishe tamaa. Na wewe pia inabidi ufanye hivyo. Kumbuka, chochote kile unachopitia kita pita. 

No comments

Powered by Blogger.