Rais wa Sevilla FC aipongeza Simba SC


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limsema kuwa lina ushirikiano wa miaka mitatu na La Liga hivyo ujio wa Sevilla kuja kucheza na Simba ni ishara kwamba ushirikiano huo ni mkubwa. 

Hayo yameelezwa leo na Rais wa TFF, Wallace Karia mbele ya Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa Simba SC na Sevilla kutoka Hispania utaochezwa hapo kesho 

"Ushirikiano wetu ni mkubwa, SportPesa imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika kusaidia maendeleo ya michezo," ameeleza. 

Kwa upande wake Rais wa Sevilla FC, José Castro amesema kuwa, "Niwapongeze sana Simba ya Tanzania kwa kuchukua ubingwa wa ligi Kuu, tumekuja kucheza na timu bora, ni heshima sana kuja Tanzania na bila shaka tutakua ni timu ya kwanza ya Laliga kuja Tanzania".

No comments

Powered by Blogger.