Ander Herrera awaaga rasmi Manchester United


Beki wa kulia na winga wa Manchester United Ander Herrera, hapo juzo alikiaga klabu hicho baada ya kandarasi yake ya miaka mitano kumalizika huku akiwashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono akiwa Manchester. 

Ander alijiunga na klabu hicho mwaka wa 2014, na kushinda mataji mawili ya Primia, kombe la FA, makombe mawili ya ligi na kombe la Ligi ya Europa. 

Herrera, mwenye umri wa miaka 29, na raia wa Uhispania, amefungia Man U magoli 20 katika michezo 189. Herrera ameichezea United mechi tisa tu msimu huu. 

Herrera alijiunga na United akitokea Athletic Bilbao ya Uhispania, na inaelezwa kuwa ataelekea kujiunga na miamba ya Ufaransa klabu ya Paris St-Germain kama mchezaji huru

No comments

Powered by Blogger.