Ronaldo afikiria haya kuhusu Man United


 Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, anafikiria timu yake itafanya yaliyofanywa na Man United dhidi ya PSG kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Juventus ya Italia dhidi ya Atletico Madrid ya Hispania. 

Ronaldo ameyasema hayo leo wakati akiongea na tovuti ya klabu kwamba wapo tayari kwa 'Come back' na anaamini watafanya hivyo kwa kutokea nyuma kwa mabao 2-0 waliyofungwa wiki kadhaa zilizopita walipoitembelea Atletico Madrid. 

"Mimi pamoja na wenzangu kwenye timu tupo tayari kwa mchezo huu mzuri na utakuwa usiku maalumu kwetu ndani ya uwanja na kwa mashabiki pia jukwaani'', amesema. 

Ronaldo amesisitiza kuwa mashabiki wanatakiwa wawaamini na kuwapa nguvu muda wote watakapokuwa uwanjani wafikirie zaidi kuwa tunafanya 'Come back'.

No comments

Powered by Blogger.